Tuesday, January 7, 2014

HOFU YA VIFO VYA WASANII YAENDELEA KUWATAFUNA MASTAA WA BONGO

HOFU ya kifo imetawala kwa mastaa Bongo ikiwa ni siku chache baada ya  habari ya utabiri wa Hussein Yahaya, ikieleza kuwa mwaka huu vifo zaidi vitaendelea kwa wasanii wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini na wanasiasa.
Aunt Ezekiel.
Risasi Mchanganyiko limepata kuzungumza na baadhi ya wasanii wa sanaa mbalimbali Bongo na kueleza maoni yao kuhusiana na utabiri huo. Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Single Mtambalike ‘Richie’ aliye msanii wa filamu ambaye alisema:
“Namwamini Mungu kwa asilimia zote, hata kama kitatokea kifo mbele yetu nina imani kitakuwa na sababu kama ugonjwa na kadhalika, siyo ghafla."
SHAMSA FORD
"Unajua ibada ndiyo kitu cha kwanza kutuokoa, mimi natoa rai kwa wenzangu wakumbuke kuomba kila mtu kwa imani yake tutashinda tu."
AUNT EZEKIEL
"Haya yanayotokea inabidi tujifunze na yaliyopita, mimi kwangu naona kama changamoto nyingine. Naahidi kumtukuza Mungu ili niepukane na balaa hili."
BEN POL
Huyu ni mkali wa R&B, yeye alisema: “Tukazane kumuomba Mungu kwa njia yoyote ile tutashinda hili jaribu."
SNURA MUSHI
Aliibukia kwenye filamu lakini sasa yupo pia kwenye muziki, akiwa ametambulishwa na kibao chake cha Majanga. Yeye alisema: “Mwaka uliopita  ulikuwa wa majanga sana, nawashauri wenzangu tukimbilie sala maana ndiyo kimbilio letu la mwisho."
-GPL


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “HOFU YA VIFO VYA WASANII YAENDELEA KUWATAFUNA MASTAA WA BONGO”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter