Friday, December 27, 2013

MENINA: ETI NITOE RUSHWA YA NGONO, MH!

MWANAMUZIKI aliyeibukia kwenye Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Menina Atick amesema licha ya kusikia kuwepo kwa baadhi ya wanaume wenye nafasi kwenye ‘game’ la muziki ambao huomba rushwa ya ngono kwa wasanii wa kike ili wawatoe, yeye atakomaa na anaamini atasimama.

 

Menina Atick.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na wimbo wake wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.

Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza nitatembea na wangapi,” alihoji msanii huyo. 

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “MENINA: ETI NITOE RUSHWA YA NGONO, MH!”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter