Friday, December 27, 2013

Diamond Platnumz kuwasomesha watoto watatu walioshinda shindano la kucheza Ngololo


 
Diamond Platnumz ni bingwa wa kuitumia karata yake ya Public Relations vizuri.  Mwezi August mwaka huu aliicheza vizuri  baada ya kumfanyia surprise mwanamuziki mkongwe wa Tanzania Muhidin Gurumo kwa kumnunulia gari kwenye uzinduzi wa video yake ya 'My Number One' uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 
Jumatano hii, staa huyo aliyekuwa ameandaa show maalum ya Christmas kwaajili ya watoto kwenye viwanja vya Leaders Club, alitisha tena baada ya kuahidi kuwasomesha bure watoto watatu walioshinda shindano la kucheza mtindo wake wa Ngololo.
 
"Management yangu ya WCB itawasomesha miaka yote waliyobakiza shuleni ikiwa ni pamoja na kuwahamishia katika shule zilizo bora zaidi,"aliandika Diamond kwenye website yake.

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “Diamond Platnumz kuwasomesha watoto watatu walioshinda shindano la kucheza Ngololo”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter