Saturday, December 28, 2013

Kijana atupwa jela maisha baada ya kumlawiti mtoto wa kaka yake mkoani Tabora..!!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Nzega, Tabora, imemhukumu Juma Lufunga (26) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.
 
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Joseph Ngomelo alisema Lufunga (26) ametiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali na hivyo kustahili kifungo cha maisha gerezani ili adhabu yake iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za aina hiyo.
 
Alisema vitendo vya ulawiti wa watoto wadogo, vimekuwa vikiongezeka kila kukicha na kusababaisha jamii ishindwe kufanya kazi zingine za maendeleo kwa hofu juu ya watoto wao kwa kuwa watu wazima wamekuwa ni tatizo hasa wanaume.
 
Kabla ya hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo Juma Lufunga akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na yeye kuwa ni mwathirika wa virusi vya Ukimwi, hata hivyo mtuhumiwa huyo alipoombwa vyeti vya uthibitisho hakuweza kuwasilisha mahakamani.
 
Awali, Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 24 mwaka 2012 majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Mwanihara, Lufunga alimlawiti mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.
 

Melito alidai taarifa ya daktari ilithibitisha unyama aliofanyiwa mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “Kijana atupwa jela maisha baada ya kumlawiti mtoto wa kaka yake mkoani Tabora..!!”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter