Tuesday, December 31, 2013

KIOJA...!! CHA KUFUNGA MWAKA: JAMAA APANDA JUU YA MNARA, AKATAA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAIS KIKWETE...

Wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa huyo. 
Wanausalama wakimshusha jamaa huyo aliyekuwa anagoma kushuka akidai mpaka Rais Kikwete afike.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo la kufunga mwaka 2013.
 

Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.
Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha.

Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi.

Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi ashijirushe na kufanikiwa kushuka naye.

(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “KIOJA...!! CHA KUFUNGA MWAKA: JAMAA APANDA JUU YA MNARA, AKATAA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAIS KIKWETE... ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter