Sunday, December 29, 2013

MATUKIO 10 MAKUBWA YALIYOTOKEA NA KUTIKISA TASNIA YA MUZIKI MWAKA 2013..!! TAZAMA HAPA



10. Kala Jeremiah Kusaini Mkataba na pepsi
Kala Jeremiah msanii mwenye tunzo 3 za hip hop kutoka Kili Music Award 2013alisaini mkataba wa miezi 6 kutoka kampuni ya PEPSI kama balozi wa soda hiyo. Kala alisema mkataba huo umempa furaha sana na amejisikia faraja sana. Sasa kala anaonekana kwenye matangazo ya pepsi na ni kitu cha kufurahisha kwenye muziki wetu.tutegemee mambo makubwa kutoka kwa kala mwaka ujao.
010.kala-jeremiah-pepsi
09 . Mabeste , Vanessa Mdee , Gosby Kuondoka BHITS
Hii ni kitu ambacho kilizua utata sana na mshangao baina ya wapenzi wa bongoflava. Mabeste ndio alikua wakwanza kutangaza hayupo BHITS  “Tatizo ni maelewano ya kibiashara kati ya mimi na uwongozi wa B”hits na si vinginevyo…..!! Akuna mtu ambaye apendi kuona faida kwenye kazi yake…!! Na kwasababu music ni kazi …Baaasi nimejaribu kutetea kazi yangu…!! Pamoja saana” alisema mabeste. Vamessa na Gosby hawakuweza kuzungumzia kwa undani kuhusiana na hali hii.
009.mabeste kuondoka bhits
08 . P-Square in Dar
” Eh – I no go lie , The things wey dey my mind , When I see you dancing, girl you got me high , And if you want to try, Gbege go dey tonight ,  Cos I’m in the mood ,  As long as you feeling the groove ,  I go deal with you ,  Personally eh ,Personal personally – ah ah ah a , Personally eh…. ” hii ndio ilikua anthem mwaka huu na pale leaders club ambapo psuare walidondosha shoo moja ya kufa mtu.P-sqare-in-dar

07. Emmanuel msuya wins Epiq Bongo Star Search
Ni mashindano yaliyokua yamejaa ushindani mkubwa sana kwa mwaka huu hasa kwa upande wa kina dada baada ya wanne kati ya 5 kufanikiwa kuingia katika top 5 lakini hiyo hakuhakikishia kwamba ushindi utabaki kwao kwani emmanuel msuya alifanikiwa kuwabwaga wote usiku wa kuamkia leo pale escape one na kitwaa taji la mshindi wa EBSS kwa mwaka huu, taji ambalo lilikua linashikiliwa na walter chilambo.
007.emmanuel-msuya-wins-bss
06 .  AY awa nominated 2 times kwenye Channel O Music Awards
Kwa mwaka wa pili sasa AY ameweza kumaintain nominations zake katika tuzo za channel o lakini cha tofauti na mwaa 2012 ni kwamba mwaka huu AY alikua nominated lakini hakupata tuzo . Hii haimshushi AY sababu kuwa recognized Africa ni jambo kubwa kwani kuna wasanii wakubwa sana hapa Tanzania kuliko AY lakini hatuwaoni kwenye tuzo kama hizi.
006---AY---Channel-O
05 . Barack Obama Amfollow Vanessa Mdee Twitter
moja ya vitu ambavyo watanzania tunajivunia ni uhusiano wetu mzuri na nchi ya marekani hasa raisi wa sasa barack obama na hata aliyepita george bush.barack obama alivyodondoka kutoka state na kuja kukutembelea hapa tanzania. moja ya kitu ambacho obama alishangwazwa nacho ni mapokezi aliyoyapata alivyokuja Tanzania na hii sasa tunaona imeanza kuzaa matunda baada ya obama kumfollow vanessa mdee kwenye ukurasa wake wa twitter.
005-.Obama-kumfollow-vanessa-mdee
04 . Diamond na Lady Jay dee Kuchukuliwa na Coke Studio
Coke Studio mwaka huu walifika africa ikiwa ni project iliyokwisha kufanyika baadhi ya nchi kama Brazil na India. Kwa upande wa Bongo Tulifanikiwa kuwaona manguli wawili wamuziki wa bongo flava namaanisha King Diamond Platnumz ambae hana dalili za kuachia his crown na Queen Lady jay dee wakiperform nyimbo mbalimbali. Hii imekua njia nzuri sana ya kuutangaza muziki wa bongo Africa na ni moja ya Breakthrough ya muziki kwa mwaka huu.
004.coke-studio-vibe-co-tz

 03 .  Adam Juma Kuacha Kufanya Music Videos
Unaweza kujiuliza kwa nini huoni video kali za Adam Juma katika soko mtu tuliemzoea katika Industry baada ya kuletea mapinduzi makubwa sana katika sanaa mpaka kufikia level ya Tzee kuweza kushindana na mataifa mengine ya Afrika.Adam Juma despite na kazi yote aliyoifanya katika muziki but still haikuweza kumlipa kiivyo na akaamua kufanya maamuzi magumu ya kukaa pembezi kwa muda akijipanga tena  na  kwasasa amejikita sana katika kufanya video za documentary na matangazo.
003.adam-juma-kuacha-kufanya-videos
02. Diamond Platnumz na Number One Movement
Baada ya adam juma kuondoka katika video productions diamond aliamua kufanya kitu ambacho hamna mtu alishawahi kukifanya, alichomoa milioni 45 na kudondoka africa kusini kufanya tunachoweza kusema video kali kuliko zote kwa hapa bongo na sio tu kwa mwaka huu bali tokea muziki huu wa bongo flava ulipoanza. Chakutegemea mwaka 2014 ni revoultion zaidi katika ulimwengu wa video hasa kama alivyosema diamond mwenyewe kuwa pesa alizotumia katika video hii ilikua ni kama investment kwasababu mwishoo wa siku mziki unalipa siku hizi sio kama zamani so pesa zote zinakuja kurudi baadae.
002.-Diamond---number-one
01. Kifo Cha Albert Mangwair
Kama wewe sio mpenzi wa bongo movies sana basi inawezekana kifo cha ngwea ndio kikawa kimekuuma zaidi. jamaa ni moja ya vichwa vya mistari na mashairi vilivyokua vimebaki. ngwea alifariki akiwa na miaka 31 tu na muziki kwake ulikua bado haujafa.  Ngwea  alifariki akiwa  chumbani huko afrika ya kusini ambapo asubuhi kulipokucha jamaa alikua amelala fofofo, rafiki zake wakajaribu kumwamsha na kumwagia maji bila mafaniko ndo ikabidi wamwahishe hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg ambapo  madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, ndipo madaktari wakatoa ripoti kuwa msanii huyo ameaga dunia.
001-.-RIP-ngwea


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “ MATUKIO 10 MAKUBWA YALIYOTOKEA NA KUTIKISA TASNIA YA MUZIKI MWAKA 2013..!! TAZAMA HAPA ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter