Thursday, December 26, 2013

MKE ADAIWA KUMUUA MUMEWE KWA KUMPIGA NA KIKOMBE KICHWANI..SOMA MKASA HUU ULIVYOTOKEA

SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amosi Joseph kwa kumpiga kwa kukombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo. 
Akisimulia  mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.

Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.

“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu.

“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.

Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana kwa jila la Christina, alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida na kumkuta kaka yake akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda mfupi polisi waliwasili na kufanya taratibu zote muhimu.

Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.

vitukovyamtaa BLOG inatoa pole familia ya marehemu na linamuomba Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amosi-Amin.
-Gpl

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “MKE ADAIWA KUMUUA MUMEWE KWA KUMPIGA NA KIKOMBE KICHWANI..SOMA MKASA HUU ULIVYOTOKEA ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter