Friday, December 27, 2013

MNENGUAJI TWANGA LIVE AKILILIA PENZI...CHEKI PICHA ALIVYOZALILIKA

Ufuska mtupu! Mnenguaji wa kiume wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Bakari Kisongo ‘Mandela’ ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada aliyetajwa kwa jina moja la Zainab.
Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.

Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na ‘fotografa’ wetu lilitokea juzi nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga ilikuwa ikivurumisha burudani ya Sikukuu ya Krismasi.
Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) akilazimisha penzi

Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onesho lake majira ya saa 9:30 usiku, mnenguaji huyo alionekana akizama kwenye Baa ya Uhuru Peak inayotazamana na Mango kisha akamwita msichana huyo ili waondoke.

Bakari Kisongo ‘Mandela’ (kushoto) kanaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada Zainab.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa karibu, kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.

Baada ya kuona hivyo, Mandela alitumia mbinu mbadala (nguvu) ambapo alimvutia mrembo huyo ndani ya Bajaj iliyokuwa imepaki eneo hilo ndipo mtafakuru ukazuka.

Huku na huku, dada huyo alipata upenyo ambapo alichoropoka na kutoka nje ambapo Mandela naye alimrukia na kuanza kumlilia huku akilazimisha mambo ya kikubwa hadharani ikiwepo ‘kudendeka’.

Hata hivyo, Mungu mkubwa kwa sababu mrembo huyo alifanikiwa kumtoka Mandela kisha akadandia Bajaj nyingine na kuondoka kwa kasi huku akimwacha jamaa na mfadhaiko.

Mashuhuda wa tukio hilo walimponda Mandela wakidai kuwa huo ni ufuska kwani kitendo alichotaka kufanya si cha kuigwa katika jamii.

Wanahabari wetu walipomtaiti Mandela kutaka kujua kulikoni kuomba mambo ya kikubwa hadharani hakuwa na la kusema zaidi ya kusikitika kumkosakosa mrembo huyo.


Read more: http://www.vitukovyamtaanews.com/2013/12/mnenguaji-twanga-live-akililia.html#ixzz2okL9kX8E

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “MNENGUAJI TWANGA LIVE AKILILIA PENZI...CHEKI PICHA ALIVYOZALILIKA”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter