
MWIGIZAJI Yvonne Cherry ‘Monalisa’ na mama yake, Suzan Lewis ‘Natasha’ wamewaacha watu midomo wazi baada ya kuonesha uhodari wa kucheza ngoma ya kizaramo.
Natasha na Monalisa wakicheza ngoma.
Mastaa hao walionesha utundu huo juzikati walipokuwa katika hafla ya mahari ya msanii mwenzao, Vanita Omary ambapo mwanamuziki Siza na kundi lake walipoimba nyimbo hizo, alianza kuinuka Monalisa kisha mama yake na kuanza kucheza kwa ustadi.Monalisa na mama yake wakicheza ngoma za Kizaramo na wageni waalikwa.
“Sikujua kama akina Mona ni wazaramo na wanajua kuicheza ngoma yao, ukweli nimewakubali wamekumbuka kabisa asili yao leo ni balaa,” alisema mama Hawa, mmoja wa waalikwa.
MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.