Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alimtaja mtoto aliyefariki kuwa ni James Stephen (1), mkazi wa Nanenane Manispaa ya Morogoro na kwamba tukio hilo lilitokea Desemba 25 mwaka huu saa moja asubuhi.
Katika tukio la pili, mtoto Veronica Chigunda (6) mkazi wa Mashambani Likwambe, Wilaya Ulanga alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Lugala baada ya kuungua moto wakati amelala kwenye nyumba anayoishi.
Kamanda Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilisababisha majeraha kwa watu wawili, akiwemo mama wa marehemu Paula Fimbo (24) na Matiasi Mahumba (1) na wote wamelazwa katika hospitali hiyo.
Shilogile alisema tukio la nne, mfugaji wa jamii ya kimasai Mela Kipara (25) mkazi wa Makole wilayani Mvomero, alifariki dunia baada ya kukatwa na mapanga na mfugaji mwenzie wakati wakitoka kunywa pombe za kienyeji.
Aidha, Mganga Machaku (35) mkazi wa Mdudu, Kilosa alikutwa ndani ya nyumba yake amekufa na mwili wake ukiwa umeharibika vibaya huku chanzo cha kifo hicho kikiwa ni kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, limejipanga kuongeza ulinzi katika kuelekea mkesha wa Mwaka Mpya.
MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.