Tuesday, January 7, 2014

BREAKING NEWZZZ..Zitto Kabwe ashinda hukumu ya kesi yake.....Mahakama yaizuia kamati kuu ya CHADEMA kujadili uanachama wake


 
LEO macho na maskio ya watanzania   hasa  wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA yalielekezwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa   alikuwa  akitoa  hukumu  dhidi  ya  Zitto Kabwe  na CHADEMA....
 
Zitto ambaye alikuwa   ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho  iliyokutana  tarehe  3  na  4  mwezi  huu  kujadili  hatima  ya  uanachama wake  wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake  ya   kupinga kuvuliwa  nyadhifa  zake  zote  za  uongozi  ndani  ya  chama  hicho... 

Akisoma  hukumu  ya  kesi  hiyo  baada  ya  kuiahirisha  jana, Jaji  wa mahakama  hiyo,Jaji Utamwa  ameridhia  pingamizi  lililotolewa  na  mh. Zitto Kabwe la  kutojadili  uanachama  wake na  kuitaka  kamati  kuu  ya  CHADEMA  au  chombo  kingine  chochote  kisijadili  uanachama  wake   hadi  kesi  yake  ya  msingi ( rufaa )  itakaposikilizwa  na  baraza  kuu  la  chama  hicho.

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “BREAKING NEWZZZ..Zitto Kabwe ashinda hukumu ya kesi yake.....Mahakama yaizuia kamati kuu ya CHADEMA kujadili uanachama wake”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter