Friday, January 10, 2014

DUH,... HII KALI KASHFA YA MAPENZI YAMWANDAMA RAIS WA UFARANSA,,,, HOLLANDE

Rais wa Ufaransa François Hollande, ametishia kuwachukulia hatua za kisheria wahariri wa jarida moja nchini humo lililochapisha taarifa za uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja muigizaji Julie Gayet.
Hollande hakukanusha madai hayo lakini alisema kuwa jarida hilo limekwenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake binafsi.
Jarida hilo, Closer,limechapisha picha kadhaa ambazo linasema zinathibitisha madai kuwa Hollande ana uhusiano wa karibu sana na Bi Gayet.Bi Gayet mwenye umri wa miaka 41 ni muigizaji msifika wa vipindi vya televisheni.
Duru zinasema kuwa ufichuzi huu umetokea wakati ambapo Hollande anakabiliwa na changamoto kadhaa katika utawala wake, ikiwemo kudorora kwa uchumi jambo ambalo wananchi wanamtarajia kulishuhughulikia.Inajulikana wazi kuwa bwana Hollande ana mpenzi mmoja tu ambaye ni mwanahabari Valérie Trierweiler.
Hollande pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa mwenzake wa chama cha kisosholidti, Ségolène Royal.
Mwezi Machi mwaka jana aliwasilisha malalamiko yake kwa kiongozi wa mashitaka Jijini Paris, dhidi ya wanablogu na wenye Mitandao ya kijamii kuwa wanaeneza uvumi.

chanzo ;bbc

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “DUH,... HII KALI KASHFA YA MAPENZI YAMWANDAMA RAIS WA UFARANSA,,,, HOLLANDE”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter