Tuesday, January 21, 2014

HAWA NDIO MAWAZIRI WALIOPIGWA CHINI BILA YA KUTEGEMEA BAADA YA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sifue kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete alitangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri ambapo ‘jiwe’ limetua kwa wasiotegemea.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sifue (kushoto) akitangaza Baraza jipya la Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo wizara tano zimepata mawaziri wapya kujaza nafasi za waliovuliwa nyadhifa zao kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza.
Waliochakuliwa ni Mathias Chikawe aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Hussein Mwinyi aliyepelekwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Lazaro Nyalandu amepewa Wizara ya Maliasili na Utalii kuiongoza.
Wengine ni Saada Mkuya Salum, ataongoza wizara ya fedha ambapo Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi mpya ni Dr. Titus Kamanyi. Naye Asha Rose Migiro ameteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba.
Manaibu mawaziri walioteuliwa na wizara zao kwenye mabano ni Adamu Malima (Fedha), Amos Makalla (Maji), Jonister Mhagama (Elimu), Janet Mbene, (Viwanda na Biashara), Kaika Telele (Mifungo, Uvuvi), Kwebe Steven Kwembe ( Jinsia na watoto) na Charles Kitwanga (Nishati).
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo amejikuta akitupwa nje ya wizara hiyo na hakuambulia nafasi yoyote.


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “HAWA NDIO MAWAZIRI WALIOPIGWA CHINI BILA YA KUTEGEMEA BAADA YA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter