Friday, January 10, 2014

MREMBO AZUA KASHESHE, KISA WIVU WA MAPENZI!...TAZAMA MAPICHA HAPA



Mrembo akizua kasheshe baada ya kutolewa nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala, Dar.

AMA kweli pombe siyo chai. Timbwili la aina yake liliibuka ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Mwananyamala jijini Dar hivi karibuni baada ya dada mmoja kuanzisha kasheshe alipomkuta mpenzi wake akiwa amekaa kimahaba na demu mwingine.

 
Mrembo akiwa mikononi mwa baunsa.

Kisa kizima kilichoshuhudiwa na paparazi wetu kilitokea majira ya saa 8:00 usiku baada ya dada huyo kwenda kujisaidia msalani na aliporudi akamkuta mpenzi wake akiwa ameinamiwa na demu mwingine kimahaba.
 
...Akitolewa nje ya ukumbi na baunsa.
Dada huyo alipomuona mpenzi wake anamsomesha demu mwingine, hakukubali akamrukia yule demu aliyekuwa akizungumza na mpenzi wake na kuwafanya wote kuanguka chini ndipo timbwili lilipoanza.

 
...Twende nje.

Hata hivyo, timbwili hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani walinzi wakiwemo mabaunsa walifanya kazi ya ziada kumtoa dada huyo ukumbini hapo huku akiwa hana viatu.


...Mrembo akitaka kurudi tena.

Hata hivyo, katika kuepusha vurugu zaidi, walinzi wa eneo hilo walimuomba mpenzi wa sistaduu huyo naye atoke nje ili wakamalize ugomvi wao kisha waende wakalale.
 
...Akizidi kukinukisha.

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “MREMBO AZUA KASHESHE, KISA WIVU WA MAPENZI!...TAZAMA MAPICHA HAPA”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter