Friday, January 10, 2014

NIPE NGONO NIKUPE SAMAKI…..!!!!–ZIWA VICTORIA

Wanawake wa Kenya wanaofanya biashara ya kuuza Samaki katika ufuo wa ziwa Victoria mjini Kisumu Magharibi mwa nchi, wanajaribu kukomesha tabia ya kujihusisha na wavuvi kingono ili wapewe Samaki bila malipo.
 
Tabia hii imelaumiwa pakubwa kwa kuchochea ongzeko la maambukizi ya HIV.clip_image002
Wakati wanawake hao wanapokubali kuwa na uhusiano wa kingono na wavuvi wanaume, basi hilo huwa kama hakikisho la kupata Samaki wa kuuza kwa kipindi kirefu.

Biashara hii inayojulikana na wenyeji kama Jaboya, ambapo mwanamke anafanya Ngono na wavuvi ili apate Samaki wa kuuza, imelaumiwa pakubwa kwa kueneza maradhi ya Ukimwi miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo ya Ziwa Victoria.

Sasa wanawake katika eneo hilo wamezindua kampeni inayolenga kukomesha biashara hiyo.

Mradi uliozinduliwa na taasisi ya utafiti wa mazingira ya Victoria, imeanza kuwapa wanawake hao maboti yao ili waweze kufanya uvuvi wenyewe.

Dan Abuto, afisaa mmoja wa shirika hilo, anasema kuwa pesa watakazolipa wanawake hao kutokana na biashara zao za Samakai, zitawaruhusu kutengeza boti zao wenyewe.

"mradi huu unalenga kushughulikia 'Jaboya' kama swala la afya ya umma , kupunguza viwango vya umasikini na kuleta usawa wa kijinsia,'' alisema afisaa huyo.

Wajane pia wanasemekana kuwa katika hatari kubwa zaidi kutokana na biashara hiyo hasa ikiwa ni jukumu lao kulisha familia zao.

Makundi ya wanawake yanasema kuwa boti hizo za thamani ya dola 920, hazitamaliza tu biashara hiyo bali pia itapunguza kuenea kwa maradhi ya Ukimwi. Ikiwa mradi huu utafanikiwa basi maambikizi nayo yatapungua pakubwa.

SOURCE: BBC SWAHILI


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “NIPE NGONO NIKUPE SAMAKI…..!!!!–ZIWA VICTORIA”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter