Wednesday, January 1, 2014

MAKUBWAAA....RAY AONA AIBU KUMKISS LULU...KISA, LINI NA WAPI?!SOMA ZAIDI HAPA.

STAA wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema alipata wakati mgumu kumpanga mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye filamu yake ambayo walipaswa kucheza kama wapenzi kwa kuhofia kumbusu

Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga cha jijini Dar hivi karibuni, Ray alisema licha ya kuwa Lulu alikuwa anastahili kuigiza katika sinema ya Woman Principle miaka kadhaa iliyopita, aliona Lulu anafaa kutokana na umakini wake lakini akaona bora amchukue Miss Tanzania namba 3, 2003, Nargis Mohammed kwa kuhofia kupata aibu ya kuoneshana malavidavi na Lulu.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Lulu alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho alikuwa mdogo sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni mtoto mdogo kama yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame nikaona bora nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.
Aliongeza kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na mvuto wa kazi yake katika jamii.


Read more: http://www.vitukovyamtaanews.com/2014/01/makubwaaaray-aona-aibu-kumkiss-lulukisa.html#ixzz2pDUGOLqy

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “MAKUBWAAA....RAY AONA AIBU KUMKISS LULU...KISA, LINI NA WAPI?!SOMA ZAIDI HAPA. ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter