Wote hawa kwangu ni miongoni mwa watu walionivutia kwenye kazi ya utangazaji (role models) na niliwatafuta kwa lengo la kutaka kushare nao hofu nilionayo sasa kwenye vipindi vya burudani katika redio nyingi za Tanzania. Hofu hiyo ni kuwa kwa mwaka 2013, vipindi vya radio vya burudani vimeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita. Kushuka kwake kunatokana na watangazaji wengi kufanya kazi kwa mazoea, kutojiandaa, kukosa vitu exclusive vya
Kwangu na kwa wengine wengi, Millard Ayo ndio mtangazaji bora zaidi Tanzania kwa sasa. Kwa miaka miwili mfululizo, 2012 na 2013, Millard amekuwa akiongoza kura za maoni za Bongo5 kuhusu mtangazaji anayesikilizwa zaidi Tanzania. Godwin Gondwe anamchukulia Millard kama mtangazaji anayejituma zaidi kuliko wote Tanzania na kwamba kama angekuwa anafanya kipindi muda sawa na yeye, basi angekuwa anampa hofu sana. Naye mtangazaji mkongwe, Masoud Masoud wa TBC Taifa, aliwahi kusema kwenye kipindi cha Mkasi mwaka huu kuwa,
Kwa muda mrefu, XXL kimeendelea kuwa kipindi namba 1 cha burudani nchini. Kama wimbo wa msanii usipochezwa kwenye XXL, basi wimbo huo una kasoro. Yeye mwenyewe B-Dozen anajiita mfalme wa vipindi vya mchana na hakuna msanii yeyote mkubwa wa Bongo ambaye hajawahi kuhojiwa na mtangazaji huyu mahiri. Kwangu mimi, B-Dozen ndio roho ya XXL ambaye kama asipokuwepo, hakuna mtangazaji anayeweza kukipa kipindi hicho ladha iliyozoeleka. Ndicho kipindi ambacho nyimbo kali za wasanii zimezinduliwa exclusively mwaka 2013. Mwaka huu B12 alitajwa kwenye orodha ya Top Ten Most ya Channel O ya watangazaji bora wa Afrika huku yeye akikamata nafasi ya 9. 3. Raheem Da Prince – The Switch, Times FM
Utangazaji wa Raheem na uelewa wake wa muziki, hunifanya nivutike sana kusikiliza kipindi chake cha The Switch kila Jumamosi. Japokuwa Madj wa show hiyo DJ D-Ommy na DJ KU ni sehemu ya kivutio cha show hiyo, ufuatiliaji wa Raheem kuhusiana na muziki wa Marekani na kwingine, hunifanya nitoke na elimu kubwa kila nisikilizapo show yake. Amekuwa akijituma sana kuchambua matukio ya muziki yakiwemo kuchambua album za wasanii wa Marekani na mambo mengine. Mwaka huu nilifurahia zaidi uchambuzi alioufanya kwa kushirikiana na Reuben Ndege aka Nchakalih, Hermy B na Miss East Africa 2012, Jocelyne Maro wa album ya Jay Z, Magna Carta Holy Grail. Sijawahi kusikia uchambuzi mkali wa muziki kama huo kwenye redio yoyoye ya Tanzania kwa miaka mingi. 4. Vanessa Mdee – The Hitlist, Choice FM
Vanessa Mdee hutangaza kipindi cha The Hitlist cha Choice FM na ndio sehemu yangu iliyosalia ya kusikiliza nyimbo mpya za Marekani ambazo kwa sasa ni nadra kuzikisia kwingine. Awali show niliyokuwa nikiitegemea kwa kusikiliza selection nzuri ya nyimbo mpya za Marekani ilikuwa ni kwenye The Cruise ya Choice FM kipindi ambacho Steve Kabuye alikuwa anatangaza bado. Napenda uchangamfu wa Vee Money kwenye show yake na uelewa mzuri wa ngoma za nje. 5. Jabir Saleh – The Jump Off, Times FM
Namchukulia Jabir Saleh aka Kuvikacha kama maktaba ya muziki wa vijana. Nadiriki kusema ni watangazaji wachache sana Tanzania wenye uelewa wa muziki wa Hip Hop kama alionao Jabir. Ukisikiliza kipindi cha The Jump Off, hakuna shaka kuwa elimu yako kuhusu Hip Hop itapanuka zaidi na kamwe huwezi kujuta kumsikiliza. 6. Sam Misago – Power Jams , EA Radio
Power Jams na XXL ndivyo vipindi vyenye ushindani zaidi kwa siku nyingi katika vipindi vya mchana. Akiwa amejipa jina ‘The Presenter’s President, Sam ni miongoni mwa watangazaji wenye mashabiki wengi mchana. 7. Bizzo – Show Time; New Chapter , RFA
Umaarufu wa Bizzo ulianzia Ebony FM, Iringa ambako alikuwa akifanya show iitwayo The Splash. Kwa sasa Bizzo ambaye jina lake halisi ni Renatus Kiluvya, ni mtangazaji wa kipindi cha Show Time cha Radio Free Africa. Kwa kiasi kikubwa amejitahidi kuliziba pengo la Kidbwoy aliyekuwa amezoeleka sana kwenye kipindi hicho. 8. Perfect Crispin – Club 10, Clouds FM
Perfect ni mtangazaji wa kipindi cha vijana hususan wa sekondari cha Club 10. Ni kipindi maarufu zaidi kwa wanafunzi wa sekondari kuliko vyote nchini na kwa kiasi kikubwa ameendelea kukimudu na kukiendesha kwa ustadi mkubwa mwaka 2013. 9. Jimmy Jamal – Daladala Beat, Magic FM
Dala Dala Beat ni miongoni mwa show kongwe kabisa za burudani nchini. Jimmy ni mtangazaji mwenye sauti nzito na mwenye uelewa mkubwa wa muziki wa ndani na nje. Napenda namna anavyofanya interview zake na uchangamfu hewani. 10. King David
Kwa wengi, King David ni jina geni kabisa. Lakini kitu kimoja cha uhakika kuhusu jamaa huyu ni kwamba ukimsikiliza lazima utamkubali na kama angekuwa anatangaza redio kubwa, kwa sasa angekuwa akicheza ligi moja na watangazaji wengi hao juu. Ana sauti nzuri na yenye mamlaka, anajua muziki wa ndani na nje na ni mbunifu. Alikuwa mtangazaji wa Uplands FM ya Njombe ambako alikuwa akifanya vipindi kama Bonge la Drive na Uplands FM Top 20 na kwa sasa amehamia kwenye kituo cha redio kipya kiitwacho Kings FM cha Njombe kitakachoanza rasmi matangazo mwakani.MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

