Hitmaker wa Pesa, Mr Blue aka Kabayser amesema tangu awe baba, maisha yake yamebadilika na haishi kama zamani tena“Nafikiri kwa mimi imenikuza zaidi,” Blue aliiambia tovutui hii. 
Mr Blue na mwanae Sameer

Mr Blue na mwanae Sameer
Hata hivyo amesema pamoja na kuwa baba, majukumu aliyonayo hayajabadilika sana japo kwa sasa amekuwa yeye binafsi na familia yake. “Kilichobadilika kwangu ni bidii kuongezeka inabidi niangalie familia yangu iandaje.”

Wahyda (mchumba wake na Blue) akiwa na mwanae Sameer
“Ni mtu kwakweli kama baba yake na mimi nafurahi,” Blue amemuongea mwanae huyo wa kiume aitwaye Sameer. “Inabidi amrithi baba yake tu kwa uchakarikaji na kila kitu.”

Katika hatua nyingine Mr Blue amesema tayari amemalizia mjengo wake na anatarajia kuhamia tarehe 1 January 2014.
MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.