Tuesday, December 24, 2013

NDOA YA THEA, MIKE YASUKWA ILI WARUDIANE

NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, Mike Sangu ‘Mike’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ iliripotiwa kuvunjika siku chache zilizopita lakini taarifa zilizotufikia zinadai kuwa, wawili hao muda si mrefu watakuwa mwili mmoja tena.
Mike Sangu ‘Mike’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, uwezekano wa wawili hao kurudiana unakuja kufuatia baadhi ya ndugu wa pande zote mbili kutofurahishwa na kusambaratika kwa ndoa hivyo kufanya jitihada za kuirejesha.
“Kuna mikakati ya kuirejesha ndoa ya Mike na Thea, baadhi ya ndugu wamekuwa wakikutana kuona nini wanaweza kufanya, ‘so’ msije mkashangaa kusikia wamerudiana,” kilidai chanzo hicho.
Katika kuonesha huenda maneno hayo yana ukweli, hivi karibuni kwenye sherehe ya msanii wa filamu Vanita Omary, ‘Vanita’ ya kuposwa na mchumba wake aitwaye Paulynus Mtenda, Mike na Thea kwa mara ya kwanza walikutana na kuchangamkiana sana huku wakiishia kukumbatiana kana kwamba hakuna kilichotokea.
Mike na Thea siku ya harusi yao.
Aidha katika sherehe hiyo Thea alisikika akimwambia mmoja wa wasanii waliokuwa hapo kuwa anampenda Mike na atabaki kuwa mume wake wa ndoa, jambo lililowaacha midomo wazi Susan Lewisy ‘Natasha’ na Yvonney Cherry ‘Monalisa’ waliokuwa karibu yao.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kutaka kuzungumza na wawili hao juu ya uwezekano wa kurudiana ambapo wote walikuwa wakichenga ila jitihada zinaendelea na lolote jipya litakalojitokeza, tutawataarifu.

-Gpl


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “NDOA YA THEA, MIKE YASUKWA ILI WARUDIANE”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter