Monday, December 30, 2013

Tume ya Warioba ( Rasimu ya pili ya katiba ) yapendekeza muungano uwe wa Serikali tatu....



Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza in ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240 .Wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora  kama  ifuatavyo:

1-lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa.

2-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
3-wabunge wasiwe mawaziri
4-kuwe na ukomo wa wabunge
5-wananchi wawajibishe wabunge
6-spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.

7-kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa.

MUUNGANO
Muungano umependekezwa uwe wa serikali tatu kutokana  na  kero  mbalimbali  zilizoko pande zote mbili. Baadhi ya kero hizo ni kama ifuatavyo:

Kero za wazanzibar
1-Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania na hivyo kutumia mwanya huo kujipatia misaada toka nje
2-mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
3-kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais

Kero za  Tanzania Bara.

1-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
2-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar  wakati wazanzibar huku Tanganyika wanaruhusiwa


Mambo mengi ya Muungano yamebadilishwa bila kufuata Katiba. HIVYO:
 

** TUME imependekeza  muundo wa muungano uwe  wa  serikali 3.

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “Tume ya Warioba ( Rasimu ya pili ya katiba ) yapendekeza muungano uwe wa Serikali tatu....”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter