Saturday, January 11, 2014

HUKU NDIKO KULITOKA TETESI ZA KIFO CHA RAIS KAGAME....WENGI WASHEREHEKEA....SOMA ZAIDI HAPA



Wakazi wa Goma walibeba jeneza bandia likiwa na Msalaba baada ya kupata taarifa hizo
Kwa masaa kadhaa Ijumaa nyakati za asubuhi, kulikuwa na fununu kuwa Rais wa Rwanda,Paul Kagame ameaga dunia na taarifa hizo zilienea hadi mji wa Goma Mashariki mwa Congo. Wengi walisherehekea baada ya kupata habari hizo.
Lakini taarifa hiyo inasemekana kutokana na ujumbe bandia kwenye Facebook.
Hapana shaka kuwa kuna uhasama kati ya DR Congo na Rwanda hasa katika eneo la Mashariki mwa DRC ambako Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa kuchochea ghasia zinazoendelea huko.

Kwa hivyo fununu zilipoanza kuenezwa kuwa Kagame amefariki, walikuwa na furaha sana.

Mamia ya watu waliandamana kwenye barabara za mji wa Goma kuelekea katika mpaka wa Rwanda kusherehekea kile ambacho baadaye kilijuliakana kuwa tu tetesi na fununu za uongo kuwa Kagame kafariki.

Hata walibeba jeneza bandia na msalaba .

Madereva barabarani walishaniglia kwa kupiga honi.

Tetetsi hizo zilipingwa vikali na serikali ya Rwanda kupitia Twitter.

Waziri mkuu wa Rwanda alijibu kwa kusema , kuwa taarifa hizo ni za kipuuzi sana huku mshauri mkuu wa Kagame pia akisema ni mambo ya kipuuzi.

Punde baada ya fununu hizo, maafisa wa serikali walichapisha picha ya Kagame kwenye Tiwtter akiamkuana na wanafunzi wageni waliotembelea nchi hiyo kutoka Marekani, ishara ya kuwa Kagame yuko hai.

Chuo hicho kimethibitishia BBC kuwa picha hiyo ni ya kweli na kuwa Kagame kweli alikutana na wanafunzi hao.

Sasa kwa kuwa Kagame yuko hai na anaendelea na kazi zake za kawaida, fununu hizo zilitoka wapi na zilianza vipi?

Wakazi wa Goma wanasema kuwa zilitokana na ujumbe kwenye facebook ambao ulitolewa kwenye mtandao bandia kuhusu taarifa za vifo. Ujumbe huo ulichapishwa na kuanza kusambaziwa watu wa Goma.

Christoph Vogel, mtaalamu wa maswala ya Goma, anasema kuwa alianza kusikia kelele za watu asubuhi na kisha kuona baadhi ya ujumbe wa Facebook ukichapishwa katika mkahawa mmoja.

Na hapo ndipo maji yalizidi unga kwani watu walianza kukusanyika wakishangilia 


Na hivyo ndivyo taarifa huibuka na kuenea ziwe na kweli au za uongo .

-BBC

MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “HUKU NDIKO KULITOKA TETESI ZA KIFO CHA RAIS KAGAME....WENGI WASHEREHEKEA....SOMA ZAIDI HAPA”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter