Ajali mbaya imetokea mda si mrefu eneo kati ya wami na segera,ajali hiyo imesababishwa na gari aina ya Noah ambayo ilikuwa inatokea Moshi mjini kuelekea Dar,Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo na pia dereva alikuwa anasinsiza hali hiyo iliyopelekea kucha njia na kuenda kuivaaa gari ya mizigo kwa mbele.
Gari hiyo ya noah pia ilikuwa imebeba watu kupita uwezo wake ambapo abiria zaidi ya kumi na mbili walikuwa ndani ya gari hiyo.Mpaka chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio hakuna aliyepoteza maisha bali watu ni majeruhi walioumia vibaya sana. Watu wakiendelea kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali hiyo tazama hapa picha za baadhi ya majeruhi na gari hiyo ya Noah iliyo pata ajali.
MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI
SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.