Friday, January 10, 2014

UKOROFI WA JOHARI KWA RAY NA CHUCHU HANS...SOMA ZAIDI HAPA

HUKU Ray na Chuchu Hans wakionekana penzi lao limepamba moto, mpenzi wa zamani wa  Ray, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuwarusha roho wawili hao baada ya kutupia mtandaoni picha inayomuonesha kidoleni amevaa pete ya ndoa.
Johari.
Wakizungumza na Ijumaa baadhi ya watu waliobahatika kuiona picha hiyo wamesema kuwa kitendo cha Johari kuweka picha hiyo ni sawa na kuwarusha roho wawili hao kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuolewa kabla ya Chuchu na Ray kufunga ndoa.
Ray na Chuchu.
“Unajua kila mtu ana njia yake ya kufikisha ujumbe, kitendo cha hivi juzi Ray na Chuchu kujiachia bila ya kificho katika Viwanja vya Leaders Club, ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Bongo Movie ni sawa na kumwambia Johari hana chake ndiyo maana na yeye ameamua kurudisha kijembe kwa staili ya kuweka picha aliyovaa pete ya ndoa ili kuonyesha kuwa yeye ataolewa ila Chuchu atachezewa tu na kutupwa,” alidai mmoja wao.
Baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa wadaku hao Ijumaa lilimuendea hewani Johari ambapo alipokea simu na kusema atafutwe muda mwingine kwani  alikuwa yupo bize.


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “UKOROFI WA JOHARI KWA RAY NA CHUCHU HANS...SOMA ZAIDI HAPA ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter