Tuesday, December 24, 2013

DIAMOND AFUNGUKA!: LULU ANABISHA SIJATEMBEA NAYE???..!!! WAULIZE WEMA NA PENNY WANAJUA!!! SOMA ZAIDI

TAA kiwango katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekanusha uvumi uliozagaa mitaani kuhusu kutoka 
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
 kimapenzi na mbabe wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
  Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Imekuwepo minong’ono ya muda mrefu kitaani kuwa, Diamond analilia penzi la Lulu lakini Diamond au Sukari ya Warembo alipoulizwa kuhusu hilo, alisema siyo kwamba analilia tu bali waliwahi kutoka (haijulikani kwenda wapi) naye, madai yaliyotupiliwa mbali na Lulu.

MADAI YA AWALI

Habari zilizotua katika meza ya paparazi wetu zinasema kwamba, wawili hao wanafanya kazi za kisanii pamoja (haikuwekwa wazi ni kazi gani kati ya filamu au muziki) lakini tatizo lililopo kati yao ni Diamond kumtaka Lulu.

Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilifunguka: “Diamond anashindwa kuelewa, tatizo yeye kila mwanamke anataka kutoka naye. Mwenzake anajua yupo kazini, yeye anataka penzi, ndiyo mzozo uliopo kati yao.

 
Wema Sepetu.

KAZI KWA DIAMOND

Paparazi wetu alimvutia waya Diamond ili kutaka kupata ufafanuzi kwa upande wake, ambapo aliposomewa maelezo yote alicheka sana kisha akasema: “Nililie penzi la Lulu? Acheni hizo... ngoja nikuambie kitu, siyo kulilia, mimi nimeshawahi kutoka naye. Nilitembea naye kishkaji tu kisha kila mmoja akaendelea na yake.

Hayo mambo yalishapita na sikutaka kuyaongelea lakini kwa sababu naona kama yanakuzwa, ndiyo maana nimeamua kuweka wazi. Kwa sasa tunaheshimiana kama kaka na dada. Kuna ugumu gani mimi kuwa naye wakati nimeshampitia?

paparazi wetu: Unasema kweli Diamond?

Diamond: Wa asilimia mia moja.

 
Penny.
paparazi wetu: Una ushahidi gani?

Diamond: Watu wanaojua hii ishu ni wawili tu; Wema (Sepetu) na Penny (Penniel Mungilwa). Niliwaeleza kwa uwazi kabisa hawa ili tusielewane vibaya. Kama huamini waulize. Hawa ndiyo niliowapa siri hii.

Paparazi wetu alijaribu kuwatafuta Penny na Wema kupitia simu zao za mkononi lakini hawakupokea.

TURUDI KWA LULU SASA

Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Lulu alimshangaa Diamond na kusema kwambasi kutoka naye tu bali hana hata kazi anayofanya naye pamoja.

Nawashangaa sana eti mimi nifanye kazi na Diamond, kazi gani sasa wakati mimi na yeye tupo kwenye fani tofauti? Muziki na  filamu wapi na wapi? Kifupi hayo madai hayana ukweli wowote na kila mtu yupo na yake,” alisema Lulu na kuongeza:

 
Lulu.
Kwanza mimi siwezi kutoka na Diamond... levo zetu ni tofauti kabisa, wala hazilingani. Mimi nilianza kutoka kabla yake, nimeanza kujulikana toka kitambo hicho nina miaka mitano sijui hata kujifuta kamasi vizuri.... hakuna ukweli wowote.”

TUJIKUMBUSHE

Diamond amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali, huku madai hayo yeye mwenyewe akiyakubali, jambo lililosababisha aitwe Sukari ya Warembo.

Mbali na orodha ndefu aliyotoka nayo Diamond, kinachovuta hisia za wengi ni uhusiano wake wa sasa, ambapo haijulikana kama yupo na Penny, Wema au wote kwa wakati mmoja!

-GP


MPENZI MSOMAJI TUPE MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI

SHARE HABARI HII KWA RAFIKI ZAKO HAPA CHINI==>>

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU BASI BOFYA "LIKE" HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK.

0 comments em “DIAMOND AFUNGUKA!: LULU ANABISHA SIJATEMBEA NAYE???..!!! WAULIZE WEMA NA PENNY WANAJUA!!! SOMA ZAIDI ”

Post a Comment

 

Mambomseto Blog Copyright © 2011 -- Template created by SKENDO TEAM -- Powered by SKENDO TEAM

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter